Posted By Posted On

SIMBA WASITUMIE LILE NENO “KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE” naandika @exaud_msaka_habari Mfumo ambao Simba waliutumia kufika hadi…

SIMBA WASITUMIE LILE NENO “KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE”

naandika @exaud_msaka_habari

Mfumo ambao Simba waliutumia kufika hadi Robo fainali ya Africa msimu ule haukuwa mfumo Rafiki kabisaaa na ulikuwa na risk nyingi, najua nikisema ilikuwa ni bahati tu mtanirarua hapa

Ila kiukweli haukuwa mfumo sahihi, mfumo wa KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE ni mfumo ambao ukizubaa kidogo tu umeliwa

Mfumo huo huo ukawacost msimu uliofuata pale simba walipotoa droo ugenini wakashangilia wakijua wanakuja kumaliza game nyumbani na ikawageuka

Msimu huu hebu wajaribu kutafuta matokeo popote walipo, wawe ugenini au nyumbani, mpaka pale wanapokutana na wagumu kabisa ndio watafute sare ugenini, hii itawasaidia kumaliza game mapema na kuondoa presha

Mimi siamini kwenye mfumo wa kila mtu ashinde zake, mimi naamini mwenye uwezo ashinde zote.

ALL IN ALL JUMATANO NI KESHO

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *