Posted By Posted On

UBORA, UWEZO WA SIMBA NA UBOVU, UDHAIFU YANGA WAONDOA KABISA UTANI WA JADI. Baada ya mechi ya Yanga na Namungo kuna tukio la ku…

UBORA, UWEZO WA SIMBA NA UBOVU, UDHAIFU YANGA WAONDOA KABISA UTANI WA JADI.

Baada ya mechi ya Yanga na Namungo kuna tukio la kusikitisha mno lilitokea.
Baada ya mechi kuna mshabiki wa Simba alimtania Shabiki wa Yanga kwa nia ya kumzogoa kama kawaida ya washabiki wa timu hizi mbili.
Mshabiki wa Simba alimwambia yule wa Yanga bado point mbili na mtazidosha kwa Azam na kazi itakuwa imekwisha. Yule mshabiki wa Yanga alichokifanya ni kumpigia kelele za mwizi. Nia ni yule mshabiki wa Simba akutane na kipigo cha wananchi wenye hasira. Kwa bahati ni kwamba yule shabiki ni maarufu na anafahamika. Hivyo kwa kuwa wananchi waliokuja kwa kasi kwa nia ya kumuadhibu kibaka walikuwa mchanganyiko ilipepelekea wengine kumtambua na kuhoji kulikoni kibaka anevaa jezi na ametoka uwanjani? Wakati huo yule shabiki wa Simba alikuwa ameshikwa na butwaa na asijue cha kufanya au nini kinaendelea kwa mshtuko. Baada ya muda na kurudi katika hali ya kawaida ndipo akajieleza alichokuwa akikifanya yeye ni utani wa mpira. Wakati yule shabiki wa Yanga aliyempigia kelele za mwizi alikuwa ameshaondoka eneo la tukio. ( Habari hii imetangazwa pia na radio Claus Fm katika kipindi chake cha michezo).
Huku ndiko tulikofikia.

Hii ilisababishwa na shabiki wa Yanga kukereka na kukosa majibu kwa shabiki wa Simba. Hivyo akaona njia ya pekee ya kujibu mapigo ndio hiyo.

Hii inatokana na mashabiki wa Yanga kukata tamaa na hawana majibu ya utani tena. Simba imewazidi kila kitu na hawaoni dalili tena ya kupambana tena uwanjani kushindana kutokana na udhaifu wa timu yao.
Hii inawapandisha hasira na kujenga chuki kwa hasira kutokana na kuwa ni watu waliokata tamaa.

Wakati msimu unaanza angalau walikuwa na matumaini bandia waliyoongopewa na viongozi wao kwamba wana kikosi cha ubingwa ila kadri muda unavyosogea taratibu wanaanza kuona maji na mafuta vinajitenga na ukweli unaanza kutamalaki. Sasa kutokana na tambo walizokuwa wamezifanya unakuta hawana chaguo bali hasira.
Hasira ambazo wako tayari kusababisha maafa ilimradi tu wapunguze machungu kwa njia hiyo.

Ukitazama mwenendo wa ligi msimu huu hakuna timu iliyobebwa kama Yanga. Aidha na marefa au vinginevyo. Lakini ni hao hao wanaoshusha lawama kwa marefa na mamlaka za mpira nchini. Hii ni mojawapo ya dalili za kukata tamaa.

Msidhani wao hawauoni ubora wa Simba au hawauoni udhaifu wa timu yao la hasha. Wanaouna sana isipokuwa hawapo tu tayari kukiri hadharani. Hii ndio inapelekea hasira zote hizi.

Niliwahi kusema ukiona Yanga wanasema Jambo la kubuni au kuzusha ili kufifisha ubora wa Simba lichunguze lina sababu. Kwa mfano wakishafanya hujuma na kujua zimefanikiwa ili kuzuia isije ikasemwa sababu ya ukweli watawahi mapema kusema Simba ina wachezaji wazee au itazusha Simba bila Chama haina lolote. Ilimradi tu wapate kichaka cha kuhalalisha uharamia wao. Kwa mfano huyu aliyetaka kusababisha maafa tukiamua kumpeleka kwenye mikono ya sheria haraka sana watakimbilia kusema na kupiga kelele kwa nguvu Simba utani umewashinda. Kuna utani wa kutaka kuuana?

Yanga wanajua kabisa hawana timu ya kupambania ubingwa na Simba kwa sasa. Na wanajua kabisa hakuna timu iliyo bora kwa sasa nchini ya kulinganishwa na Simba. Hivyo ili kuhalalisha angalau uharamia wa njia za panya kutafuta ushindi wanatumia nguvu kubwa kudanganya Uma kwamba Simba ni timu ya kawaida na haina kiwango cha tofauti na nyingine. Ila isivyo bahati namba zinawaumbua. Simba imefunga mabao 28 ambayo ni karibu mara mbili ya timu inayofuatia. Timu bora siku zote hupimwa kwa uwezo wa kufunga magoli. Na hata huko kuzuia tofauti kati ya ukuta Simba , Yanga, na Azam ni goli moja. Wakati Simba imeruhusu kufungwa goli tano wakati Yanga na Azam wameruuhusu goli nne kila mmoja. Hivyo ukipima tu hapo utagundua timu ipi ni bora kuliko nyingine. Kupoteza mchezo timu zote bora duniani hutokea zikapoteza mchezo ila huwa haiondoi kwamba TIMU YENYE KUKAMIA HUSHINDA MECHI ILA TIMU BORA HUTWAAA TAJI.
Yanga wanajua Simba inakwenda kutwaa ubingwa kwa Mara ya nne mfululizo na hili ndio linasababisha wawe na hasira na kutafuta uhasama badala ya utani.

MASHABIKI WA SIMBA KUWENI MAKINI JAMAA WANA HASIRA KUTOKANA NA UBOVU NA UDHAIFU WA TIMU YAO.
( Jicho la tatu la Mgalilaya).

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *