Posted By Posted On

COASTAL UNION YAZINDUKA NA KUICHAPA IHEFU SC 1-0 MKWAKWANI, MBEYA CITY NAO WASHINDA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAO pekee la Salum Ally dakika ya 16 limetosha kuipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Ushindi unaofuatia kipigo cha 7-0 kutoka kwa mabingwa watetezi, Simba SC kinaifanya Coastal Union ifikishe pointi 15 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya 10.
Uwanja wa Chuo cha Ushirika, bao pekee la beki Pato Ngonyani dakika ya pili likaipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.


Naye Kibu Dennis akaibuka shukaa wa Mbeya City baada ya kufunga bao pekee dakika ya 68 katika ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *