Posted By Posted On

Photos from SokaPlace’s post

NYONI,KISU CHA BUTCHER KINAISHA NA MAKALI YAKE..

Na Octa Ayubu Jr.

Masaa 24 ya siku ya Tarehe 7 mwezi mei mwaka 1988 huenda Ni miongoni mwa masaa yaliyokuwa yamebeba tabasamu zito kwenye paji la uso la mzee Edward Nyoni.Kwani miongoni mwa masaa hayo 24 ya Tarehe 7 alipokea zawadi kubwa maishani mwake pale Alipopata mtoto wa kiume aliyembatiza jina la Erasto Edward Nyoni.

Erasto nyoni Ni miongoni mwa wachezaji wachache wenye heshima kubwa kwa soka la ukanda wa afrika mashariki.Kwa Majibu wa passport ya kusafilia inatuambia ifikapo mei 7 mwakani Erasto atakuwa anakata keki ya kutimiza miaka 33.

Alianza kufahamika alipojiunga na Rolling stone na baadae AFC ikamtambulisha rasmi katika ramani ya soka la Tanzania.Siyo Simba Wala Yanga zilizostuka Kama Kuna miongoni mwa wachezaji viraka bora pale AFC mpaka watu wa Vital’O kutoka Burundi walipoinasa sahihi yake.

Kitendo cha Nyoni kusaini nje Tena kwenye moja ya klabu kubwa pale Burundi Bila kupita Simba au Yanga liliwastua watu wengi wakaanza kumfuatilia,ndipo mabosi wa Azam fc wakampata akitokea Vital’O.Misimu 7 ndani ya jezi za waoka mikate Azam fc Alionyesha uwezo mkubwa mno wa kucheza soka Huku makocha wakinufaika mno na Nyoni kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya tano uwanjani.

Uwezo wa Nyoni uwanjani umekuwa Ni mkubwa mno licha ya umri wake kuonekana kusogea Lakini ufundi ulioweka kambi ndani ya miguu yake umegoma kufanya usaliti kwasababu ya kumbukumbu ya kiapo kilichofanyika ndani ya tumbo kabla ya kuzaliwa.

Licha ya majeruhi madogo madogo bado Nyoni ameendelea kuwa Bora pale anaporejea kutoka kitandani.Nyoni siyo mchezaji anayehitaji mechi mbili au tatu za mashindano ndipo upate ubora wake,ila mazoezi tu ya pamoja yanatosha kumpata Nyoni halisi katika mechi yake ya Kwanza tu akitokea kitandani kuuguza majeraha yake.

Amekuwa miongoni mwa wachezaji waandamizi timu ya taifa Huku akicheza kwa ubora mkubwa na kuonyesha tofauti yake na wachezaji chipukizi Kama Mwamnyeto na Abdallah kheri ambao tunawatazamia kuja kuunda safu ya ulinzi baadae katika Timu ya Taifa.

Ukongwe na uzoefu tu havitoshi kumfanya Nyoni tuendelee kumuabudu,Lakini Nidhamu ya ndani na nje ya uwanja inamsaidia Sana kuwa Bora.Ukaribu wao ulipo huenda ukawasaidia zaidi Kennedy Juma na Ibrahim Ame Kama wataamua kumtumia vizuri mkongwe huyu ambaye Kwangu naona Hana tofauti na Kisu Cha buchani ambacho kinaisha chuma Lakini siyo makali yake.

Ninachoamini tuna misimu zaidi ya mitatu ya kumfaidi Nyoni katika ubora huu mkubwa.Misimu mitatu pale Simba kafanya makubwa mengi ambayo huenda yanakosa airtime kutokana na ubora wa Timu nzima.lakini Timu ya taifa lazima Nyoni aonekane kwa ukaribu kutokana na makosa mengi yanayofanywa na Timu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *