Posted By Posted On

Azam FC watoa ufafanuzi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wao mpya Mpiana Monzinzi: Kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni ku…

Azam FC watoa ufafanuzi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wao mpya Mpiana Monzinzi:

Kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wetu mpya, @platine40 Mpiana Monzinzi, kutoka FC Lupopo ya DRC.

Taarifa hiyo inayoonekana imetolewa na FC Lupopo, inamlalamikia Monzinzi kuondoka bila ruhusa na kusaini mkataba na klabu nyingine (sisi Azam FC) bila wao (FC Lupopo) kuwa na taarifa.

UKWELI WA HILI
Kimsingi sisi Azam FC, tumemnunua mchezaji huyu kutoka klabu ya Academic Club Rangers, ambayo ndiyo inayommiliki.

Huko Lupopo alienda kwa mkopo ambao ulitakiwa kukamilika Juni mwaka huu.

Lakini ACR ambao ndiyo wamiliki halali, wametuuzia mchezaji huyo kwa vielelezo vyote.

Ni jukumu la ACR na Lupopo kuwasiliana na kuliweka sawa swala hili.

Tumewasiliana na ACR kupitia Rais wao, Lambert Osango Nsenga, ambaye kimsingi ndiyo mmiliki halisi wa mchezaji huyu.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa DRC humilikiwa na watu, na hao watu huwapeleka wachezaji hawa kwenye vilabu mbalimbali kwa mkopo ili kutengeneza soko.

Bwana Lambert amesema hawajawapelekea Lupopo taarifa rasmi, lakini tusiwe na wasiwasi, watafanya hivyo baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tunawaomba mashabiki wetu mfurahie kwa amani sikukuu ya Krisimasi na Mwaka mpya, mkiwa na uhakika kwamba Mpiana Monzinzi ni mchezaji wetu halali.

Tunawaomba mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi, kila kitu kiko kwenye udhibiti.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *