Posted By Posted On

MERRY CHRISTMAS WANA WA ADAM . Mwenyezi Mungu atujaalie Baraka na Upendo, furaha iwe zawadi yetu ya milele wanangu wa soka . Wak…

MERRY CHRISTMAS WANA WA ADAM
.
Mwenyezi Mungu atujaalie Baraka na Upendo, furaha iwe zawadi yetu ya milele wanangu wa soka
.
Wakati nafurahia siku hii nimetumia muda kupumzika ila kila nilipo sinzia na kuamka huu mchezo wa soka uliniteka akili yangu, kuna vitu niliviwaza na kufurahi, picha ya Messi hapo juu inaelezea mood yangu ya leo
.
Ila dah kuna muda nilijikuta nmeweka kichwa chini nilivyomuwaza Mesut Mustapha Ozil na Arsenal, nikashika kalamu nikaandika kitu
.
Nikaingia Youtube nikasafiri kidigitali mpaka Harare nakarudia highlights za Mnyama na Fc Platnum, nilipomuona Larry Bwalya nikanyong’onyea nikashika kalamu nikaandika makala kichwa chake cha habari ni DHAMBI YA KARIAKOO DERBY NA HUKUMU YA ABUNUASI
.
Inabidi kesho niwape makala moja kati ya hizo mbili
.
Ila bado kuna kitu kikaja kichwani kikanifanya nitabasamu kama Messi hapo kwenye picha, nilikumbuka ya kuwa Boxing day ya kesho kuna utamu wa hatari na suprise za kutosha, nikakumbuka ya kuwa EPL pale kila boxing day uwa tunapata suprise ya matokeo, nahisi kuna mkubwa anakufa kesho 😂😂
.
Baada ya kuwaza mengi nikaikumbuka sauti ya Jaydee “Jide” na nyimbo ya “Mawazo”
.
Sema nini, Sio kesi, Kesho nayo siku wana familia, sikukuu ikawe yenye furaha na baraka, tusisahau kusali na kushukuru Mungu, na kufurahi pia
.
Bado naendelea kupokea mialiko ya pilau hata kipolo 😁
.
📃
.
Feliz Navidad

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *