Posted By Posted On

Photos from VIWANJANI LEO’s post

Wakati huu ambao Lionel Messi akisherekea msimu wa sikukuu ya Christmas huku akiwa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyofunga Idadi mkubwa zaidi ya Magoli 644 akiwa Katika Klabu moja, kampuni moja ya bia aina ya Budweiser iliamua kusherekea sikukuu ya Christmas kwa kuwapatia chupa za Bia Kutoka kiwandani kwao kwa kila kipa Ambaye amewahi kufungwa goli Dhidi ya Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi kwenye rekodi yake ya mabao 644 kwa Barça

🙌 Makipa wote 160 Tofauti Walipokea Idadi ya chupa kulingana na Idadi ya magoli ambayo wamewahi kufungwa na nyota huyo wa soka Duniani, kila chupa ambayo golikipa husika aliipokea ilikuwa imeandikwa namba ya goli ambalo alifungwa, ikiwa na maana kama alikufunga goli la 20, 21,34. 60 basi utapokea chupa zenye namba za magoli ambayo alikufunga.

Diego Alves na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Iker Casillas ndio waliopokea Idadi kubwa ya chupa ikiwa na maana kwamba ni makipa wanaoongaza kwa kufungwa Magoli mengi zaidi na Lionel Messi, Alves aliipokea chupa 21 huku Casilas akipokea chupa 17

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *