Posted By Posted On

Hesabu ya Kylian Mbappe ilienda sawa na hatua za miguu yake. Anaandika @jacksonsillo SOMO la Hesabu “Hisabati” ni gumu kuliko …

Hesabu ya Kylian Mbappe ilienda sawa na hatua za miguu yake.

Anaandika @jacksonsillo

SOMO la Hesabu “Hisabati” ni gumu kuliko masomo yote, hii ni dhana iliyojengeka kwa watu wengi Duniani (Wakubwa kwa wadogo). Mara nyingi huwa hivi kwa sababu somo lenyewe linahitaji mazoezi mengi, jambo ambalo huwashinda wengi pia.

Achana na Hisabati ya Shuleni, tuna ile ya soka. Katika hili huwa tunatazama takwimu na kiwango cha mchezaji kwenye mechi husika, huwa zinapanda na kushuka.

Kupanda, hii inachagizwa zaidi na mazoezi mengi ya kutosha “Binafsi na ya timu” pamoja na nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Kushuka, hii huchagizwa na mazoezi hafifu, majeraha ya mara kwa mara na hata utovu wa nidhamu ambao hupelekea kutoaminiwa ndani ya kikosi cha kwanza.

Huyu hapa Mbappe anayezidi kuyafanya yale yasiyotegemewa na wengi katika mchezo tajika wa soka, kwanza tuzitazame hizi namba.

Akiwa na Monaco tangu mwaka 2015-2017 kwenye timu ya wakubwa ametumika katika michezo 53 akifunga mabao 20.

Ndani ya miaka 4 aliyodumu PSG hadi leo ukijumlisha na mwaka 1 aliyocheza kwa mkopo tayari ametumika katika michezo 97 akifunga zaidi ya mabao 65.

Hadi sasa 2020/2021 kunako LIGUE 1 anaongoza kwenye orodha ya ufungaji akiwa na mabao 16, kunako UEFA ana mabao 5 nyuma ya Alvaro Morata (6), Neymar Junior (6), Marcus Rashford (6) na Erling Halaand (8).

Lakini pia alihusika pakubwa mno pale ambapo Taifa lake Ufaransa lilipofanikiwa kutwaa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Katika kiwango bora sana, hakika ni mwenye harufu ya NUNI..!

Ni huyu huyu Mbappe ambaye miaka 9 iliyopita (2012) alitemwa na Chelsea kwenye timu ya Vijana akionekana kuwa hana uwezo wala kipaji cha kujiunga hapo.

Utakumbuka wakati huo alikuwa na umri wa miaka 13, wakati wengi wakidhania kuwa ameshafeli kumbe yeye alikuwa akiendelea kukokotoa hesabu ambayo sasa inaenda sawa sawia na hatua za miguu yake.

Ameshacheza kwa mafanikio mengi makubwa sana tena kwa muda mfupi tu akiwa na umri mdogo, hata hili la kufunga HAT TRIK mbele ya Barcelona tena Nou Camp si dogo kabisa.

Acha tuendelee kufaidi hesabu za MBAPPE zenye majibu sahihi ya kile kilichojificha kwenye mlinganyo tata.

AHSANTENI .
#sokaplaceupdates

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *