Posted By Posted On

KUELEKEA MCHEZO WA LEO MO AMWAGA MILIONI 400 MWARABU AFE Simba chini ya mwekezaji bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’, imewatangazia wa…

KUELEKEA MCHEZO WA LEO MO AMWAGA MILIONI 400 MWARABU AFE

Simba chini ya mwekezaji bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’, imewatangazia wachezaji na benchi la ufundi motisha ya Sh milioni 400 kama wataifunga Al Ahly ya Misri leo Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika ambazo SA tumezipat kabla ya mchezo huo, viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba inayoongozwa na Mo, jana Jumatatu alikutana na wachezaji wa timu kambini kwao Ndege Beach nje kidogo ya jijini Dar es Salaam.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kikao hicho kilikwenda sambamba na kula chakula cha jioni na lengo ni kuwapa morali wachezaji hao katika kuhakikisha wanapata ushindi.

Katika kikao hicho ilitolewa ahadi ya wachezaji kama wakifanikiwa kupata ushindi, kama unakumbuka mchezo dhidi ya AS Vita walipewa Sh 150 Milioni baada ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 walioupata, hivyo sasa wamepandishiwa mzigo hadi Sh 400Mil kama wakifanikiwa ushindi na hiyo ni kutokana na ukubwa wa timu wanayocheza nayo,” alisema mtoa taarifa huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *