Posted By Posted On

NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE FAINALI ZA AFCON U20 BAADA YA KUCHAPWA 3-0 NA MOROCCO MAURITANIA

TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, AFCON U20 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi C jana Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott nchini Mauritania.
Mabao ya Morocco yalifungwa na viungo El Mehdi Moubarik dakika ya nne kwa penalti, Mohammed Amine Essahel dakika ya nane na mshambuliaji Ayoub Mouloua dakika ya 13.
Tanzania inamaliza na pointi moja nyuma ya Ghana iliyoaliza na pointi nne sawa na Gambia waliomaliza nafasi ya pili, wakati Morocco imeongoza kwa pointi zake saba.
Ghana imefuzu Robo Fainali za AFCON U20 kama mshindi wa tatu bora zaidi ya washindi wa tatu wa makundi A na B.

RATIBA YA ROBO FAINALI AFCON U20

Alhamisi Februari 25, 2021
Saa1:00 usiku
Cameroon U20  –  Ghana U20
Saa 4:00 usiku
Burkina Faso U20  –  Uganda U20
Ijumaa Februari 26, 2021
Saa 1:00 usiku
Morocco U20  –  Tunisia U20
Saa 4:00 usiku
Jamhuri ya Afrika ya Kati. U20  –  Gambia U20

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *