Posted By Posted On

UNACHAGUA NINI?? MIMI NACHAGUA HIKI HAPA.. . Kitabu changu kinaniambia, kikosi cha Al Ahyl kina thamani ya zaidi 75 bilioni shil…

UNACHAGUA NINI?? MIMI NACHAGUA HIKI HAPA..
.
Kitabu changu kinaniambia, kikosi cha Al Ahyl kina thamani ya zaidi 75 bilioni shilingi, kikosi cha Simba thamani yake ni bilioni sita shilingi tu. Hii ni kama kitabu changu hakijahakikiwa karibuni.

Ni tofauti kubwa sana kati yao lakini Simba hawakukubali hiyo ‘tofauti ionekane uwanjani’. Ni kazi kubwa sana imefanywa na Simba kuanzia kwenye menejimenti kisha benchi la ufundi mpaka uwanjani. Angekuja mgeni leo, ‘angefikiri Al Ahyl wamevaa jezi nyekundu’. KAZI KUBWA SANA WAMEFANYA SIMBA.

Siujui mshahara wa Didier Gomes Da Rosa, lakini naufahamu mshahara wa Pitso Mossimane. ‘Ni kifo na usingizi’. Lakini Didier hakukubali hilo lionekane uwanjani. Mbinu kubwa sana ametumia Didier. Kazi kubwa sana ameifanya Didier. Hail to that man.

Jina la Walter Bwalya ni zito na maarafu kuliko la Joash Onyango. Lakini Onyango anajua jinsi ya kulizuia lisimlemee. Nadhani sasa ni muda wa Onyango kumtoa Bwalya mfuko wake wa kushoto na Ajayi mfuko wake wa kulia. Labda Bwalya na Ajayi wataamka asubuhi na kuangalia kama Onyango yupo uvunguni mwa vitanda vyao🤠. Yule ndio stopper Ochieng.

Nasikia Elshenawi ndiyo golkipa anayeheshimika zaidi Misri. Nasikia ni golkipa bora zaidi anayecheza Afrika. Sijui atalala na nani leo lakini Najua atashtuka usiku na kuuliza kama bado Luis Miquissone anamshambulia. What a hit Luis?? What a hit! Yale magoli Ulaya wanalipia milioni kuyatazama, sisi tumeliona kwa buku tatu tu.

Mkikutana na kocha Didier huko, muambieni ampe Aish likizo ya wiki nzima huko. How did he save that one?? How did he?? Magolkipa wakubwa wanakata mikono kwenye mechi kubwa. Vile kama Salum Aish.

Mwisho tuweke takwimu sawa, Al Ahyl ya Pitso Mossimane imepoteza mechi mbili tu mpaka sasa. Moja ipo huko Ulaya, ni bingwa wa huko na bingwa wa dunia. Mwingine ni nani?? Waite Wanalunyasi. Waite wekundu wa Msimbazi. Dar es Salaam is red yoh!

Nauliza tena Unachagua nini?? Mimi nachagua kuwasifia Simba. KAZI KUBWA SANA WAMEFANYA SIMBA. KAZI KUBWA SANA IMEFANYIKA! Tanzania is red yoh!
.
✍@deo_mwanasoka

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *