Posted By Posted On

Timeline Photos

ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema kwa sasa yupo fiti kurejea kikosini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Hivi karibuni, Mwambusi aliachia nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga baada ya kupata matatizo ya kiafya. Nafasi yake imechukuliwa na Nizar Khalfan.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwambusi alisema: “Nimefanyiwa upasuaji kwenye jino na tayari nina wiki mbili, naendelea vizuri, sisikii maumivu tena kama mwanzo.

“Naona kuna mabadiliko na nitarudi tena hospitali Jumatano ili kujua maendeleo zaidi, endapo nitakuwa sawa naweza kurejea Yanga.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *