Posted By Posted On

Omari Kaya afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Namungo FC pamoja na wachezaji wawili wa klabu hiyo; Hamisi Mgunya na Lucas Kikoti wa…

Omari Kaya afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Namungo FC pamoja na wachezaji wawili wa klabu hiyo; Hamisi Mgunya na Lucas Kikoti wamerejea nchini Tanzania baada ya kuzuiwa nchini Angola kutokana na kukutwa na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19.

Afisa huyo na wachezaji hao wa Namungo walizuia nchini Angola siku 16 zilizopita baada ya klabu yao kwenda nchini Angola kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya mtoano dhidi ya klabu ya CD de Agosto. Sekeseke la vipimo hivyo lilipelekea mechi hiyo na ya marudiano kufanyika Tanzania ambapo Namungo walifanikiwa kuvuka hatua hiyo na kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki na kufika hatua hiyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *