Posted By Posted On

KWANINI TUNAIZUNGUMZA SANA SIMBA KULIKO YANGA KIPINDI HIKI naandika @exaud_msaka_habari Kwa namna yoyote Simba haiwezi kutoka…

KWANINI TUNAIZUNGUMZA SANA SIMBA KULIKO YANGA KIPINDI HIKI

naandika @exaud_msaka_habari

Kwa namna yoyote Simba haiwezi kutoka kwenye mawazo ya Waandishi, wachambuzi, Magazeti, Radio, na watu wa mitandaoni kipindi hiki

Simba wapo kwenye nafasi ambayo usipowazungumza sasa huenda ukajiona kuna kitu hutendi haki. Sababu ni hizi

1. Simba wapo Club Bingwa afrika, wanaiwakilisha Tanzania na Afrika mashariki yote

2. Simba anaongoza Kundi lake lenye Bingwa wa afrika

3. Kikosi cha wiki cha Club Bingwa Simba imetoa wachezaji wawili

4. Goli Bora la Wiki afrika limetoka Simba

5. Kipa wa Simba ametajwa na kurasa rasmi za CAF kama kipa bora kwa wiki ya kwanza ile

6. Simba ameweka historia ya kuwa club ya pili kuwafunga Al ahly baada ya Buyern

7. Simba ameweka historia ya kuwafunga AS Vita kwao

8. Lakini kubwa zaidi Simba tangu aje CEO mpya wamekuwa na matukio makubwa ambayo lazima yajadiliwe mfano Simba Super Cup, Visit Tanzania, Aina ya usajili wao, nk

Hizo ni sababu kadhaa za uwanjani zinazofanya simba ijadiliwe sana kipindi hiki, sjataja zile nyingine kama Soka wanalotandaza kwenye Ligi, Idadi ya magoli wanayofunga kwenye mechi zake za ndani, Aina ya Kocha waliyenaye, Aina ya Msemaji wao, Uwekezaji wao kwa sasa, na nyingine nyingi

Kwahiyo Sishangai kuona Simba ikijadiliwa sana sasa, sio Tanzania tu hata afrika inawajadili, tuache watambe

ALL IN ALL KWELI TUJADILI UJENZI WA HOSTEL UNAOANZA NA CHUMBA KIMOJA KWELI?

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *