Posted By Posted On

HITIMANA AMTAJA BARNABAS CHANZO KUTIMKA MTIBWA Kocha Hitimana Thierry ameweka wazi sababu za kuondoka Mtibwa Sugar kuwa ni kuto…

HITIMANA AMTAJA BARNABAS CHANZO KUTIMKA MTIBWA

Kocha Hitimana Thierry ameweka wazi sababu za kuondoka Mtibwa Sugar kuwa ni kutoelewana baina yake na Msaidizi wake Vincent Barnabas.

Hitimana amesema amevumilia kwa muda mrefu ilikuwa aondoke tangu mwezi Disemba sababu ilikuwa haijulikani nani Kocha Mkuu sababu kulikuwa hakuna maelewano.

Raia huyo wa Burundi ameenda mbali zaidi kwa kusema alishtakia kwa uongozi mara kadhaa na kuahidiwa kuwekwa chini kulimaliza suala hilo lakini hakuna kilichofanyika.

“Nimeamua kuondoka nimekuja nyumbani kwanza kukaa na familia, tangu nimeenda Mtibwa sikuwa na maelewano na Barnabas.

“Ili kuinusuru Mtibwa lazima mimi niondoke sababu Barnabas alikuwa anawaambia wachezaji akisimama yeye ndio timu inashinda sasa huoni kama huo ni mpasuko,” amesema Hitimana.

Cc @boiplusmedia

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *