Posted By Posted On

NAMUNGO FC WALAZIMISHA SARE YA 1-1 NHUMBANI NA IHEFU MECHI YA LIGI KUU LEO MAJALIWA

WENYEJI, Namungo FC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu SC ya Mbarali, Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa. Ruangwa mkoani Lindi.
Ihefu ya kocha Zubery Katwila ilitangulia kwa bao la Raphael Daudi dakika ya 23, kabla ya Ibrahim Mkoko kuisawazishia Namungo inayonolewa na Hemed Suleiman ‘Morocco’ dakika ya 61.
Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 19, ingawa inabaki nafasi ya 10, wakati Ihefu sasa ina pointi 21 za mechi 25 na inasalia nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 18.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbeya City imelazimishwa sare ya bila mabao na Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mbeya City ya kocha Mganda, Mathias Lule inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 24 ingawa inabaki nafasi ya 16, wakati Kagera Sugar ya kocha Mkenya, John Barasa inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 25, japokuwa inabaki nafasi ya 13.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *