Posted By Posted On

TFF: Mwakalebela Anafurahisha Genge . Shirikisho la mpira wa miguu nchini ‘TFF’ limefafanua kuwa adhabu aliyopewa Makamu Mwenye…

TFF: Mwakalebela Anafurahisha Genge
.
Shirikisho la mpira wa miguu nchini ‘TFF’ limefafanua kuwa adhabu aliyopewa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye upande wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.
.
“Kama ambavyo taarifa ya adhabu ilivyosema, na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea.” amesema Ndimbo
.
“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu.”
.
“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana yake umekwenda kama mtazamaji mwingine.”
#sportskitaatv #Talentonlinetv

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *